bomoabomoa kwa wakazi wa kijiji cha ng'ong'ono  kilichopo katika mkoa wa Dodoma imewaacha hoi. watu hawa wame bomolewa nyumba zao za biashara( maduka) pamoja na vibanda vidogovidogo vya biashara kisa ni kujenga ndani ya mpaka wa chuo kikuu cha dodoma (udom) katika kitivo cha elimu.
Awali kabla ya hapa wananchi hao walikua wamepewa taarifa hii tokea mwaka jana ila hawakubomoa majengo na vibanda hivyo ,hivyo ikapelekea kutoamini baada ya kuletewa tangazo lingine mwaka huu mwezi wa tano mwanzoni kuhusu kubomolewa kwa majengo haya.
Aidha madhara mengine yaliyoambatana na ubomoaji huo ni kwa upande wa wanachuo hiki ambao wengi wanatokea katika kitivo cha elimu, ambao walikua wameweka bili ya vyakula katika baadhi ya migahawa hiyo ambayo ilibomolewa na kuwaladhimu wanachuo hao kwenda kuwatafuta wamiliki wa migahawa hiyo mahali walipo ili wapate kufikia mwafaka kuhusu mwendelezo wa bili zao.
pia baadhi ya wakadhi wa eneo hilo wamejikuta wakibaki bila makazi baada ya kuvunjiwa nyumba zao na kuwaladhimu kuomba msaada kwa majirani zao.
kwa mengine mengi tutakua tunakuja kadri tupatavyo nafasi.
usikose kutembelea blog hii ili upate habari kemkem kila siku. 

Comments

Popular posts from this blog

MAUAJI KIBITI AZIDI KUENDELEA JE SHIDA NINI ???

Ndalichako mkali balaa hebu soma hii ujionee mwenyewe alichokifanya