Posts

SULUHISHO LA MAUAJI YA PWANI NI KU.........

Image
Friday, May 26, 2017 Sakata la Mauaji Pwani: CCM yataka viongozi wenye dhamana Wajiuzulu Chama cha Mapinduzi (CCM) kimelaani vikali mauaji ya baadhi ya viongozi, raia na askari polisi, waliouawa kwa kupigwa risasi katika wilaya za Rufiji, Kibiti na Mkuranga mkoa wa Pwani, na kutoa pole kwa familia zilizoguswa na mauaji hayo. Akizungumza na waandishi wa habari  jana jijini Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey  Polepole alisema chama hicho kwa niaba ya wananchi kinawataka viongozi wenye dhamana na usalama wa wananchi kujitafakari, huku akisisitiza kuwa ikiwa mauaji hayo yataendelea, chama hicho kitaielekeza serikali kuwachukulia hatua. “Sasa imetosha, yeyote mwenye dhamana ajitafakari.Hatupendi kusema hali hii ikiendelea watu wawajibike, ingawa kuwajibika kwa sababu ya watu kupoteza maisha ni ustaarabu wa kiungozi. Viongozi wote na wenye dhamana mchukue hatua, sitaki tufike pahala niseme, CCM tutaielekeza serikali kuchukua hatua...

USIPITWE NA HABARI MAGAZETIN

Image
Saturday, May 20, 2017 Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya May 20

STAR TV YAAMUA KUVUNJA UKIMYA KHUSU ZUIO LA MAKONDA..TEF YATOA KAULI

Image
Saturday, May 20, 2017 Tamko la TEF baada ya Star Tv kutangaza kufanya mahojiano na Makonda

HATIMAYE MEYA WA ARUSHWA AACHIWA HURU KUTOKA POLISI NAE AN HAYA YA KUNENA...

Image
Saturday, May 20, 2017 Meya wa Arusha Afunguka Maneno Mazito baada tu ya kuachiwa na Polisi leo Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro amesema kuwa ataelekeza fedha zote za rambirambi kwa wafiwa  badala ya kuzipeleka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo. Aidha amehoji ni kwanini fedha za rambirambi zilizochangwa kwaajili ya msiba wa wanafunzi 32, walimu wawili na dereva mmoja kuchotwa Sh.milioni 1.5 kupelekwa kama rambirambi katika msiba wa bwana na bibi harusi waliosombwa na maji Kata ya Sambasha iliyopo Wilayani Arumeru kama pole. Meya, Lazaro aliyasema hayo leo Jijini Arusha wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuachiliwa na Jeshi la Polisi leo majira ya saa 12:30 asubuhi kisha kwenda ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kaskazini. Amesema fedha hizo za rambirambi zitakazochangwa na watu mbalimbali kisha kuletwa kwake kama Meya wa Jiji la Arusha, atazielekeza kwa wafiwa moja kwa...

DUUH HAYA BHANA MAGUFULI NDOIVO ANAKABIDHI NGAZI YA UENYEKITI

Image
Saturday, May 20, 2017 Rais Magufuli akabidhi Uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Rais Museveni wa Uganda Rais John Magufuli leo (Jumamosi) amemkabidhi rasmi uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kwa Rais Yoweri Museveni.   Muda mfupi kabla ya kumkabidhi nafasi hiyo, Rais Magufuli ambaye alikuwa mwenyekiti wa EAC kwa miaka miwili amewashukuru wanachama wa jumuiya hiyo kwa kumuamini na kumpa nafasi hiyo miezi michache baada ya kuingia madarakani.   “Mliniamini mkanichagua licha ya kuwa madarakani kwa muda mfupi,”amesema Rais Magufuli ambaye aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa EAC, mapema mwaka jana.   Rais Magufuli amesema anaimani na Rais Museveni kuwa atafanya kazi nzuri kutokana na uzoefu wake. “Yaliyonishinda kuyatatua, atayatatua yeye (Rais Museveni),”amesema.   Mara baada ya kukabidhiwa nafasi hiyo, Rais Museveni ambaye sasa ni mwenyekiti wa EAC amesema atahakikisha anatumikia nafasi hiyo kwa nguvu na uwezo ...
Image
Saturday, May 20, 2017 Watanzania 11 Watiwa Mbaroni Afrika Kusini Wakituhumiwa Kumbaka Mwanamke Mjamzito Wanaume 11 ambao ni raia wa Tanzania wamekamatwa na Polisi na kufikishwa Mahakamani wiki hii  Johannesburg Afrika Kusini . Radio na Mtandaoni Johannesburg wiki hii kumeripotiwa kuwa kosa lililofanya Wanaume hao 11 kukamatwa na Polisi ni kumbaka Mwanamke mjamzito mwenye umri wa miaka 22 aliyekua akitoka kazini saa kumi na moja alfajiri. Mwanamke huyo alikua akitoka kazini na Mfanyakazi mwenzake ambaye ni Mwanaume ambapo ghafla walivamiwa na kundi la Wanaume wenye silaha za moto na wakamvuta Mwanamke huyo kabla ya kumpiga Mfanyakazi mwenzake ambae baadae alifanikiwa kutoroka. Baada ya Mfanyakazi huyo kutoroka aliwapigia simu Polisi na wakafanikiwa kuwahi eneo la tukio na kukuta Wanaume hao wakimbaka kwa zamu Mwanamke huyo mwenye ujauzito wa miezi mitatu. Polisi wapatao kumi waliingia kwenye jengo tukio lilikofanyika na kumuokoa Mwana...